|
YAZID BIN MUAWIYAH BIN ABU SUFIYAN
Kimeandikwa Na:
Sayyid Murtaza Rizvi
Babu yake
Yazid, Abu Sufiyan ni miongoni mwa wale waliosilimu pasina budi ili
kulinda mali zao na maisha yao katika Fat-hu Makka. Kauli zake
zathibitisha wazi kutokumuamini Mtume (s.a.w.w.). Alimwambia Abbas “O
Abbas! Kwa hakika mpwao amepata ufalme mkubwa” Abbas alimjibu “Ole wako!
Huu si ufalme! Huu ni Utume.” Rejea: (Tarekh Yakubi J. 2 Uk. 59.).
Baba yake
Yazid, Muawiyah ni miongoni mwa wale waliompiga vita Imam Ali (a.s.)
katika vita ya Swiffin. Pia aliamrisha makhatibu kumlaani Imam Ali
(a.s.) katika khutba za Ijumaa na Idd kwa muda wa miaka 80. Rejea: (Sahih
Muslim J. 4 Uk. 1284 - 1285, na Hayatu Omar bin Abdul aziz Uk.
252.).
Bibi yake
Yazid, Hinda ndiye aliyekula Ini la Sayyidina Hamza katika vita vya
Uhud.Yazid alifuata nyayo za babu, bibi na baba yake katika imani na
matendo. Nae wazi wazi akiimba mashairi ya kufru akisema: “Laibat
Hashim bil mulki-falaa khabarun ja’a wala wahyun nazal” yaani: Banu
Hashim walicheza mchezo wa kupata ufalme: kwa hakika hakukuwa na habari
yoyote (kwa Mungu) wala wahyi wowote ulioteremshwa.” Rejea: (Tarekh
Tabari J. 13 Uk. 2174.).
Yazid
alitangaza wazi wazi kutomuamini Mtume (s.a.w.w.) na ujumbe wake.
Alichezea shere Imani ya siku ya malipo, alidhihaki sala, ulevi ulikuwa
kinywaji chake, kamari kwake ni kawaida. Alikuwa akizini mpaka na mama
zake wa kambo na shangazi zake. Rejea: (Maruuju Dhahab J. 3 Uk. 77.
na Al-Bidaya wan-nihayah J. 5 Uk. 746.).
Katika
kipindi chake Yazid alifanya uharibifu mkubwa katika Dini. Jeshi
lilivamia miji mitukufu ya Makka na Madina. Aliwaua wasomaji wa Qur’an
700 na pia aliwaua mamia ya Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na
waliwazini wanawake kwa maelfu na kuuchafua msikiti wa Mtume
(s.a.w.w.). Mji Mtukufu wa Makka ulizingirwa na jeshi la Yazid na moto
mkali uliwashwa kwenye Al-Kaaba na sehemu ya Al- Kaaba kuvunjika. Rejea:
(Muruuju Dhahab J.3 Uk. 81.).
|