|
MANENO YA HEKIMA YA IMAM SHAFI (R.A.)
1. Katika
mambo yenye kunikesheza na kuzifanya nyeupe nywele zangu (yaani mvi) ni
huzuni na misiba ya kilimwengu.
2. Huzuni
yangu imenirudia na moyo wangu unahuzuni jicho langu halifumbi wala
usingizi siujui.
3. Kwa
sababu ya Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) ulimwengu mzima ulitetema,
Majabali na Milima ilikaribia kuyeyuka.
4. Ni nani
atakaye mfikishia Hussein ujumbe wangu na hata nyoyo
zachukia.
5. Hussein
aliuliwa shahidi pasi makosa yoyote na kanzu yake ikapakazwa wekundu.
6.
Twamuombea rehma Mtume katika ukoo wa Hashim na huku twawaudhi wanawe,
hakika jambo hilo ni lenye kushangaza
7. Ikiwa
dhambi zangu ni kuwapenda watoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) basi ni
dhambi ambazo sitatubia
|