|
Uislamu Ni nini?
Mwandishi:
Hujjatul
Islam wal Muslimeen Al-Haj Sayyid Muhammad Rizvi
Uislamu ni
Dini inayowaongoza Waumini wake katika kila nyanja ya maisha yao. Ni
mfumo wa maisha.
Uislamu ni
mwongozo au Wahyi ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu kupitia Mtume Adamu,
Nooh, Abraham, Mussa na Issa (Yesu).
Uislamu
uliletwa kwa Mwanadamu kupitia kwa Mtume Muhammad. Uislamu ni
“mwongozo” kwa maana kwamba umeletwa kuhakiki mafunzo yalioletwa kupitia
kwa Mussa na {Yesu}Issa.
Uislamu ni
Dini inayoelezea maana na kusudio la maisha yetu katika Ulimwengu huu.
Uislamu unatuongoza sisi katika kukidhi kusudio kwa kutengeneza
mazingira ya uelewano baina yetu, Muumba wetu na Wanadamu.
Yafuatayo ni
baadhi ya mambo ya msingi katika Uislamu.
MWENYEZI
MUNGU NI MMOJA NA PEKE YAKE
Uislamu ni
Dini inayoitakidi Mungu mmoja. Uislamu unatufundisha kuwa Mungu ni
mmoja na ndiye Muumba wa Ulimwengu. Hili ndio jiwe la msingi la Uislamu
na msingi huu umeelezewa katika usemi maarufu usemao: “Hapana Mola
isipokuwa Allah” (Allah ni jina la Kiarabu la Mola jina hili
linatamkwa “Al-lah”).
Kuamini
Mungu inatufungamanisha sisi na utangu (mwanzo) wetu na kutuongoza
katika maisha yetu yote. Imani yetu katika Mungu mmoja inatuashiria
kuwa mwanadamu hatakiwi kuabudia kitu chochote au Binadamu yeyote katika
Ulimwengu huu.
Kwa
kufundisha kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja kwa Wanadamu wote, Uislamu
hueneza nadharia ya udugu na usawa katika jamii ya Wanadamu wote wanao
uhusiano ulio sawa kwa Mwenyezi Mungu. Qur’an {kitabu kitakatifu cha
Kiislamu} inasema:-Yeye Allah ni (Mungu) mmoja tu. Al-lah ni Mwenye
kukusudiwa na Wahitaji wote. Hakuzaa wala Hakuzaliwa. Wala hakuna hata
mmoja mfano Wake. {Sura 112}.
KUSUDIO LA
MAISHA
Maisha yetu
katika ulimwengu huu yanayo makusudio maalum, na sio matokeo ya ajali ya
asili wala sio adhabu kwa kula tunda la mti uliokatazwa na Mwenyezi
Mungu. Tupo hapa kutokana na mipango yake Allah. Maisha ya hapa
Duniani ni majaribio, dhidi ya maisha ya Peponi baada ya maisha ya hapa
{Duniani}. Mwenyezi Mungu hakutuumba tu kwa ajili ya maisha ya miaka
michache hapa Duniani. Kuumbwa kwa ajili ya maisha ya hapa Duniani tu
ingekuwa ni mzaha uliochezwa baina ya Muumba {Allah}na jamii ya
Wanadamu. Muhammad Mtume wa Uislamu amesema “Hujaumbwa ili ufe na
kupotea bure ila {lakini}umeumbwa kwa ajili ya maisha ya milele.
Kulingana na
Imani ya Kiislamu Kituo cha mwisho cha mwanadamu ni maisha ya hapo
baadae {Akhera}. Mwisho, wanadamu wote watafufuliwa na wataulizwa siku
hiyo kuhusu matendo yao walipokuwa hapa Duniani. Maisha ya Akhera
yatakuwa ni maisha ya milele. Hata hivyo, maisha ya peponi au adhabu
{Jahannam}itategemea ni vipi tutayatumia maisha yetu hivi sasa.
Kumsaidia mwanadamu afikie lengo hili Mwenyezi Mungu amewaleta Manabii
na Mitume mbali mbali ili kuwaongoza. Muhammad ni Nabii wa mwisho na
Uislamu ni Wahyi wa mwisho wa ujumbe wa Allah uliokamilika.
HADHI YA
MWANADAMU KATIKA UISLAMU
Kiumbe
Bora:
Mwanadamu ni
kiumbe bora cha Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu amesema: “Na hakika
tumewatukuza Wanadamu na tumewapa vya kupanda barani na baharini, na
tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewatukuza kuliko wengine katika
wale tuliowaumba, kwa utukufu ulio mkubwa kabisa”. {Qur’an 17:70}
Tumezaliwa
bila dhambi:
Uislamu unatufunza kuwa kila mwanadamu huzaliwa bila dhambi {takatifu}
hakuna kizazi kinachobeba mzigo {madhambi} ya mababu {wahenga} zao.
Allah {s.w.t.}anasema; Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwingine {kila
mtu atachukua jukumu la dhambi zake mwenyewe} Surah 35 Ayah 18. Kila
mwanadamu anazaliwa akiwa safi (bila dhambi:) akiwa tayari kuupokea
ujumbe wa Al-lah. Ni mazingira ya kijamii na kifamilia yanayomtoa
mwanadamu nje ya ujumbe wa Allah.
Uwajibikaji:
Uislamu pia unasisitiza suala la majukumu na uwajibikaji kwa
wanadamu-kila mmoja anawajibika kwa vitendo vyake mwenyewe. Ingawa
Uislamu unatufunza kuwa A-l lah{s.w.t.}amesha weka tayari mwenendo wa
maisha yetu na wakati wakifo, hii haina maana kuwa hata vitendo vyetu
vimepangwa na Allah {s.w.t.}. Hakika tupo huru na vitendo vyetu, hivyo
tunawajibika navyo. Mwenyezi Mungu ametoa mwongozo tu, kwa mwanadamu
kujua lipi jema na lipi baya. Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika sisi
tumemuongoa {tumembainishia} njia {zote mbili hizi, kuwa hii ndio ya
kheri na hii ndio ya shari}. Basi {mwenyewe tena}atakuwa mwenye
shukurani au awe mwenye kukufuru, {kukanusha}. {Qur’an Surah 76:3}.
Uraia
{Ukabila}:
Uislamu unakataa unyanyasaji wa kikabila kwa misingi yoyote ile. Uislamu
unafundisha misingi ya udugu na usawa miongoni mwa waumini wake. Allah
{swt}anasema wazi wazi:
“Enyi watu!
Kwa hakika tumekuumbeni {nyote} kwa {yule} mwanamume mmoja; Adamu} na
{yule yule} mwanamke {mmoja; Hawwa}. Na tumekufanyeni mataifa na
makabila {mbalimbali} ili mjuane {tu basi;sio mkejeliane}.” Allah
anaendelea kusema; Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya
Mwenyezi Mungu ni yule amchae Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini
Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, mwenye habari {za mambo yote}. {Qur’an 49:13}.
Jinsia:
Hata jinsia haiwezi ikamweka mtu katika ubora. Katika Uislamu Wanawake
ni Wanadamu kama wanaume. Hawa tengwi kwa misingi ya jinsia yao;
isipokuwa kwa misingi ya Imani na vitendo vyao. Miaka 1400 iliyopita
Qur’an imeeleza wazi ujumbe wa Allah kuhusu suala hili. Zipo Aya nne
zinazoelezea suala hili, hapa nanukuu Aya moja: “Na watakao fanya
vitendo vizuri, wakiwa wanaume au wanawake hali wao ni wenye kuamini
basi hao wataingia Peponi wala hawata-dhulumiwa hata tunda ya kokwa ya
tende”. {Qur’an 4:124}
Hivyo hakuna
tofauti katika daraja au ubora wa utu wa mwanamume au mwanamke mbele ya
Uislamu.
Ubora pekee
unaopatikana hapa unahusu kiwango na upeo jinsi Uislamu ulivyopokewa na
mwanamume na mwanamke. Katika Uislamu, mwanamume na mwanamke wapo sawa
katika haki, lakini usawa huo haubaki hivyo katika vitendo vyao.
Uislamu unaamini kuwa mwanamume na mwanamke wako sawa, lakini hawafanani
kw vitendo vyao. Uislamu naangalia tofauti ya majukumu yao katika
Jamii kuwa sio makubwa wala madogo lakini yenye yenyekutegemeana.
UISLAMU DINI
YA AMANI
Uislamu ni
dini ya Amani. Hii inathibitishwa hata katika jina “Isalmu”. Jina
lenyewe {“Islamu ni neno la Kiarabu} Jina “Islamu” ni neno la Kiarabu
la amani “Salam” yote mawili yanatokana na asili moja “Salima”.
Waislamu
wanafundishwa kusalimiana kwa kusema “Salamun alaykum-amani iwe juu
yako”. Sala za kila siku pia humalizia kwa maneno hayo. Katika
Uislamu, miongoni mwa majina ambayo Mwenyezi Mungu huitwa ni “Salam”
ikiwa na maana ya “amani”.
Hata hivyo
mtu lazima atambue kuwa amani haiwezi kupatikana kwenye sehemu tupu
{isiyo na kitu}. Lazima iunganishwe na haki. Mtu anaweza kupata amani
tu, katika misingi ya haki. “Haki” maana yake kuweka kila kitu katika
nafasi yake. Iwapo mtu ataanza kuweka vitu katika sehemu isiyohusika
ataukera utulivu wa jamii na kuvunja amani. Uislamu huhifadhi amani
katika nyanja mbili.
1. Amani
ya Mtu binafsi:
Mtu hupata
amani yake binafsi kwa kuwa mtulivu na kuwa na uwiano wa mwenendo
{matamanio na hasira} na matendo ya kiroho.
Nguvu ya
kiroho ya mwanadamu haina utulivu uliojitosheleza; inayo uwezo wa kukuwa
na pia kuvia. Mwenyezi Mungu anaapa kwa moyo wa mwanadamu na anasema:-
“Bila shaka amefaulu aliyeitakasa {nafsi yake}Na bila shaka amejihasiri
aliyeiviza nafsi yake” {Qur’an 91:10}.
2.
Amani na Wanadamu wengine: Uislamu umesisitiza kwa nguvu zote juu
ya haki ambazo watu wengine wanazo juu ya wengine. Uislamu unahubiri
amani katika jamii kwa kuwafunza na kuwataka Waumin wake kutekeleza haki
zao baina yao. Katika Uislamu wokovu haupatikani kwa kutekeleza Haki za
Allah tu. Muumini atatakiwa kutekeleza haki za Wanadamu wengine pia.
Kwa bahati mbaya kutokana na matukio ya Mashariki ya kati kwa muda wa ¾
ya karne, Uislamu umepewa jina na vyombo vya habari kuwa ni Dini ya
ghasia {mapambano}, katika miaka ya karibuni neno “Uislamu” limekuwa
miongoni mwa sifa za “Ugaidi”.
Katika hali
hii kwanza lazima mtu atambue kuwa matukio ya Mashariki ya Kati yanaweza
kufahamika vema tu kwa msaada wa kihistoria wa vita kuu ya kwanza ya
eneo hilo, hususan ahadi zilizotolewa na Wazungu kwa Waarabu. Pili
hakuna mtu mwenye akili timamu angethubutu mwenyewe kuilaumu Dini ya
Kiislamu kwa matendo maovu ya wale wanaojiita Waislamu. Hii ni kama
kusema Kanisa Katoliki linazua ghasia na Ugaidi kwa sababu ya shughuli
za Jeshi la “Irish Republican”.
Je,
unafahamu kwamba:-
* Kila watu
watano Duniani, mmoja ni Mwislamu?
* Waislamu
walio wengi sio Waarabu wa raia wa Uarabuni?
* Wapo
Waislamu million 4.6 U.S.A.?
* Uislamu
ni Din inayo enea kwa haraka zaidi U.S.A.?
* Je! huu si
wakati muafaka kwako kujikurubisha na Uislamu?
Ewe Allah
tuangazie juu yetu mwanga wa Elimu na Utuondoe kutoka kwenye giza la
ujinga.
Ijaze mioyo
yetu kwa Elimu na Hekima.
Ijaalie
Elimu yetu iwe ya manufaa kiroho. Tujaalie mafanikio katika kujua na
kuuhami Uislamu. AMEEN!
|