|
IMAM HUSEINI BIN ‘ALI (A.S.)
Mwandishi:
Hujjatul Islam wal Muslimeen Al-Haj Sayyid Muhammad Rizvi
Jina: Huseini.
Kuniyah:
Abu ‘Abdillah.
Lakabu:
Sayyidu ‘sh-Shuhadã.
Baba:
‘Ali bin Abi Tãlib
Mama:
Fatimah bint wa Mtume.
Kuzaliwa:
3 Shabani 4 A.H. Madina
Kufariki:
10 Muharram 61 A.H. Karbala, Iraq.
1.
Kuzaliwa na maisha yake ya mwanzo:
Imamu
Huseini (Sayyidu ‘sh-Shuhadã / Bwana miongoni mwa mashahidi), mtoto wa
pili wa’Ali na Fatimah, alizaliwa mwaka wa 4 A.H., na baada ya kaka yake
Imamu Hasani kuuliwa shahidi akawa Imamu kwa amri ya Allah (kupitia kwa
Mtukufu Mtume) na wosia wa kaka yake.
Imamu
Huseini siku zote alikuwa na kaka yake wakati wa uhai wa mtume na Imamu
‘Ali; alichangia katika matukio muhimu zaidi ya kipindi hicho. Alikuwa
bega kwa bega na kaka yake wakati wa kipindi kigumu cha Uimamu wa kaka
yake. Uimamu wake mwenyewe ulikuwa wa kipindi cha miaka kumi
2. Utawala
wa Mu’awiyah:
Imamu
Huseini aliishi chini ya masharti magumu ya uonevu na mateso. Hii
ilitokana na ukweli kwamba awali ya yote sheria za dini na kanuni
zimepoteza uzito na sifa zake nyingi na sheria za serekari ya Bani
Umayya zimepata mamlaka kamili na uwezo. Pili, muawiyah na wasaidizi
wake walitumia kila njia inyowezekana kuwaweka kando na kuwaondoa nje ya
njia Ahlul Bayit wa Mtume na Shi’ah, na hivyo, kufutilia mbali jina la
‘Ali na familia yake. Na juu ya yote, Mu’awiyah alitaka kuimarisha
msingi wa ukhalifa wa mtoto wake, Yazidi, ambaye kwa sababu ya ukosefu
wake wa kanuni na aibu alipingwa na kundi kubwa la Waislam. Kwahiyo, ili
kuzima upinzani wote, Mu’awiyah alichukuwa njia mpya na kali zaidi, kwa
nguvu na kulazimika, Imamu Huseini aliishi siku hizo na kuvumlia kila
aina ya uchungu wa akili na kiroho na mateso kutoka kwa Mu’awiyah na
wasaidizi wake – mpaka katikati ya mwaka wa 60 A.H. Mu’awiyah alifaliki
na mtoto wake Yazidi akachukua nafasi yake.
3. Yazid
Adai Bay’ah
Kiapo
cha utii (bay’ah) ilikuwa ni desturi ya zamani ya Kiarabu ambayo ilikuwa
ikifanywa katika mambo muhimu sana kama yale ya ufalme na utawala. Wale
ambao walikuwa wakitawaliwa, na hususani wale wanaojulikana sana
miongoni mwao, watatoa mkono wa kiapo, makubaliano na utii kwa mfalme au
malikia wao na kwa njia hii wataonyesha kuunga kwao mkono vitendo vyake.
Kutokubaliana na hayo baada ya kula kiapo cha utii kulichukuliwa kama
aibu na kujivunjia heshima kwa mtu, ni kama kuvunja mkataba baada ya
kuwa umekwisha sainiwa rasimi, ilikuwa ikuchukuliwa kama jinai ya wazi
kabisa. Kwa kufuata mfano wa Mtukufu Mtume, watu waliamini kwamba kiapo
cha utii kama kikitolewa kwa utashi na sio kwa nguvu, hubeba uzito na
mamlaka.
Mu’awiyah
aliwataka watu wanaojulikana sana miongoni mwa watu kula kiapo cha utii
kwa mwanae Yazid, lakini hakuliweka ombi hili juu ya Imamu Huseini.
Alimuambia Yazid katika wosia wake wa mwisho kwamba kama Huseini
akikataa kula kiapo cha utii kwako, basi aliache hilo lipite kimya
kimya, na habari yenyewe aipuuze, kwani alielewa kwa usahihi kabisa
majanga ambayo yangetokea kama suala hili lingelazimishwa kwa nguvu.
Lakini kwa utovu wake wa dini na ukatili wake, Yazid alipuuza ashauri
wa baba yake na punde tu baada ya kifo cha baba yake alimuamrisha gavana
wa Madina mambo mawili, amma amlazimishe Imamu Huseini kula kiapo cha
utii au apeleke kichwa chake Damascus.
Baada ya
gavana wa Madimna kumjulisha Imamu kuhusu matakwa haya ya Yazid, Imamu
alikataa kukubaliana na matakwa hayo ya Yazid, na ilipofika usiku wa
manane aliondoka yeye na familia yake kuelekea Makka. Alichukua hifadhi
katika sehemu takatifu ya Mungu ambayo katika Uislamu ni sehemu rasimi
ya kukimbilia na usalama. Kadhia hii ilitokea mwishoni mwa mwezi wa
Rajabu na mwanzoni mwa mwezi wa Shabani mwaka wa 60 A.H. Imamu Huseini
alikaa uhamishoni mjini Makka karibu miezi minne. Habari hizi zilienea
pote katika ulimwengu wa ki-Islamu. Kwa upande mwingine watu wengi ambao
walikuwa wamechoshwa na dhulma za utawala wa Mu’awiyah na zaidi
kutoridhishwa wakati Yazid atakapokuwa Khalifa, waliwasiliana na Imamu
na kumuelezea imani yao kwake. Kwa upande mwingine mafuriko ya barua
yalianza kufurika, hususani kutoka Iraq na haswa kutoka mji wa Kufa,
wakimkaribisha Imamu aende Iraq na akubali utawala wa wengi kule pamoja
na lengo la kuanzisha harakati za kukabiliana na dhulma na unevu. Kwa
namna ilivyo, hali kama hiyo ilikuwa hatari mno kwa Yazid.
Imamu
Huseini aliendelea kukaa mjini Makka mpaka wakati wa msimu wa hijja
wakati Waislamu kutoka ulimwenguni pote wlipoanza kumiminika kuingia mji
Makka kwa makundi kwa ajili ya kutekeleza ibada ya hijja. Imamu
aligundua kwamba baadhi ya wafuasi wa Yazid wameingia Makka kama
mahujaji wakiwa wamepewa amri ya kumuua Imamu wakati wa ibada ya hijja
na huku wakiwa wamebeba silaha ambazo wamezificha ndani ya ihram zao.
Imamu
alifupisha ibada ya hijja na kuamua kuondoka. Katikati ya mkusanyiko
mkubwa wa watu, alisimama na katika hutuba fupi alitamka kwamba
anaondoka kuelekea Iraq. Katika hotuba hii fupi, vile vile alitangaza
kwamba angeuliwa shahidi na akawataka Waislamu kumsaidia katika
kulifikia lengo ambalo analo katika mawazo yake na kutoa maisha yao
katika njia ya Allah (swt). Siku iliyofuatia aliondoka yeye na familia
yake na kikundi cha masahaba zake kuelekea Iraq.
Imamu
huseini alikuwa ameamua kutokula kiapo cha utii kwa Yazid na alielewa
vizuri sana kwamba tauawa. Alikuwa anafahamu ya kwamba kifo kilikuwa
hakiepukiki mbele ya jeshi lenye nidhamu ya woga la utawla wa Bani
Umayyah, ukiungwa mkono kama ilivyo na baadhi ya sekta, uporomokaji wa
kiroho, na ukosefu wa utashi miongoni mwa watu, haswa katika nchi ya
Iraq. Baadhi ya watu maarufu wa Makka walisimama upande wa Imamu Huseini
na wakamuonya juu ya hatua ambayo anataka kuichukuwa. Lakini alijibu
kwamba alikataa kula kiapo cha utii na kutoa uthibitisho wake kwa
serikali ya dhulma na madhalimu. Aliongeza kusema kwamba alijua kwamba
popote atakapoelekea au kwenda angeuliwa. Ataondoka ili kulinda heshima
ya nyumba ya Allah (swt) na kutoruhusu heshima hii kuharibiwa kwa damu
yake kumwangwa pale.
4.
Kuelekea Karbala
Wakati
akiwa njiani kuelekea Kufa na ikiwa ni siku chache tu toka aondoke
Makka, alipokea habari kwamba wakala wa Yazid katika Kufa amemuua
muwakilishi wa Imamu katika mji huo na ambaye vile vile alikuwa mmoja wa
watu walioamua kumuunga mkono, mtu anayejulikana sana mjini Kufa. Baada
ya vifo vyao, miguu yao ilifungwa na kuburuzwa mitaani. Mji pamoja na
vitongoji vyake uliwekwa chini ya uangalizi mkali, na wanajeshi wasio
idadi wa adui waliwekwa tayari kumsubiri Imamu wamshike. Ilikuwa hakuna
njia nyingine kwake isipokwa kuendelea mbele na kukikabili kifo. Hapa
ndio sehemu ambapo Imamu alielezea uamuzi wake imara wa kuendelea mbele
akauawe shahid; na hivyo aliendelea na safari yake.
Takriban
kilometa sabini kutoka Kufa, katika jangwa linaloitwa Karbala, Imamu na
msafarea wake walizunguukwa na jeshi la Yazid. Kwa muda wa siku nane
walikaa katika hali hii wakati ambapo ukawa mwembamba na idadi ya jeshi
la adui iliongezeka. Hatimaye Imamu pamoja na familia yake na idadi
ndogo ya masahaba wake walizunguukwa na jeshi la askari sabini elfu.
Wakati wa siku hizo Imamu aliimarisha msimamo wake na akafanya uchanguzi
wa mwisho wa masahaba zake. Ulipoingia usiku aliwaita masahaba zake na
katika hotuba fupi alieleza kwamba hakuna chochote mbele yetu isipokuwa
kifo na shahada. Aliendelea kusema kwamba kwa vile maadui walikuwa na
haja na yeye tu binafsi, angewatoa katika majukumu yote haya hivyo
kwamba mtu yeyote anayetaka anaweza kutoroka katika giza hili na kuokoa
mnaisha yake. Kisha aliamrisha taa zizimwe na wengi wa wale waliojiunga
kwa manufaa yao walitawanyika na kuondoka. Ni wale wachache tu ambao
waliipenda haki na Banu Hashim walibaki.
Kwa mara
nyingine tena Imamu aliwakusanya wale ambao wamebaki na akawaweka katika
mtihani. Waliwahutubia masahaba zake na jamaa wa Banu Hashim, akisema
tena, maadui wanamtaka yeye tu binafsi. Kila mmoja anaweza kunufaika na
giza hili la usiku na kujiepusha na hatari. Lakini safari hii masahaba
waaminifu wa Imamu kila mmoja alijbu kwa njia yake kwamba hata mara moja
hawtapotoka kutoka njia ya haki ambayo Imamu alikuwa kiongozi na kamwe
hawatamuacha peke yake. Walisema watailinda familia yake mpaka tone la
mwisho la damu yao, na ilimradi muda wanaweza kubeba panga zao.
Katika siku
ya tisa ya mwezi wa Muhrram maadui walimfanyia Imamu changamoto ya
mwisho ya kuchagua kati ya “kiapo cha utii au vita”. Imamu aliomba
kuahirishwa hilo lli kwamba aweze kufanya ibada usiku ule na kuwa katika
uwamuzi imara wa kuingia katika vita siku inayofuata.
Katika siku
ya kumi ya Muharram mwaka wa 61/680 Imamu alijipanga mbele ya maadui
pamoja na kundi dogo la wafuasi wake, watu si chini ya tisini ambao ni
masahaba zake, thalathini ambao ni baadhi ya asikari wa jeshi la maadui
ambao walijiunga naye wakati wa usiku na siku ya vita, na watoto wa
familia ya Banu Hashim, ndugu zake, wapwa, na binamu zake. Siku ile
walipigana kuanzia asubuhi mpaka pumzi yao ya mwisho, na Imamu na vijana
wa kibanu Hashim na masahaba wote waliuawa mashahidi. Mwiongoni mwa wale
waliuliwa ni watoto wawili wa Imamu Hasani ambao mkubwa alikuwa na miaka
kumi na tatu na mdago alikuwa na miaka kumi na moja; na mtoto wa miaka
mitano na mtoto mchanga anaye nyonya wote wa Imamu Huseini.
Baada ya
vita kwisha, jeshi la adui liliteka nyara familia ya Imamu na kuchoma
mahema yake. Waliikatakata miili ya mashahidi. Waiiacha uchi na kuiacha
bila kuizika. Kisha wakaondoka na jamaa ya familia yake, wote walikuwa
ni wanawake na wasichana wsiojiweza, sambamba na vichwa vya mashahidi,
mpaka Kufa. Miongoni mwa wafungwa alikuwepo jamaa watatu wa kiume; mtoto
wa miaka ishirini wa Imamu Huseini ambaye alikuwa anaumwa sana na hawezi
kutembea, aitwaye ‘Ali bin Huseini, Imamu wa nne; mtoto wake wa miaka
minne, Muhammad ibn ‘Ali, ambaye alikuja kuwa Imamu wa tano. Maadui
waliwachukuwa wafungwa mpaka na kutoka pale mpaka Damascus mbele ya
Yazid.
5.
Matokeo ya Karbala:
Matekeo ya
Karbala, kutekwa kwa wanawake na watoto wa Ahlu ‘l-Bayit wa Mtukufu
Mtume, kuchukuliwa kwao wafungwa kutoka mji mwingine mpaka mji mwingine
na hotuba zilizotolewa na binti wa ‘Ali, Zainabu, na Imamu wa nne ambaye
alikuwa miongoni mwa wafungwa, iliwaabisha Banu Umayya. Unyanyasaji huu
wa familia ya Mtume ulitangua propaganda ambayo Mu’awiyah aliifanya kwa
miaka mingi. Suala hili lilifikia ukubwa kiasi kwamba Yazid alilazimika
kukana hadharani na kulaani vitendo vya mawakala wake.
Tukio la
Karbala lilikuwa ni kipengele kikubwa katika kupinduliwa kwa utawala wa
Banu Umayah ingawa matokeo yake yalicheleweshwa. Vile vile huimarisha
mizizi ya Ushia. Miongoni mwa matokeo yake ya mara moja ilikuwa ni maasi
na vurugu zilizo changanyika na umwagaji damu ambao uliendelea kwa muda
wa miaka kumi na mbili. Miongoni mwa wale ambao walikuwa ni wahusika
katika kifo cha Imamu, hakuna hata mmoja ambaye aliweza kuepuka kisasi
na adhabu.
Mtu ambaye
anachunguza kwa ukaribu historia ya maisha ya Imamu Huseini na Yazid na
hahi ambayo ilikuwepo wakati ule, na akachambua sura hii ya historia ya
ki-Islamu, atakua hana shaka yoyote kwamba katika mazingira hayo
kulikuwa hakuna hiari mbele ya Imamu Huseini bali kuuliwa tu. Kula kiapo
cha utii kwa Yazid kungelimaanisha kuonyesha hadharani kuutweza Uislamu,
kitu ambacho kilikuwa hakiwezikani kwa Imamu, kwani Yazid hakuonyesha
kutokuuheshimu Uislamu tu na maamrisho yake bali vile vile alionyesha
kwa vitendo hadharani usafihi. Akikanyaga chini ya miguu yake misingi
yake na sheria zake. Wale waliokuwa kabla yake, ingawa walipinga sheria
za dini, siku zote walifanya hivyo kwa kutumia pazia la dini, na angalau
mwanzoni waliheshimu dini. Walijifaharisha kwa kuwa masahaba wa Mtukufu
Mtume (saw) na watu wengine wa dini ambao watu waliwaamini.
Kutokana na
hili inaweza kuhitimishwa kwamba, madi ya baadhi ya wafasri wa matukio
haya ni ya uwongo wakati wakisema kwamba ndugu hawa wawili, Hasani na
Huseini walikuwa na ladha mbili tofauti na kwamba mmoja alichangua njia
ya amani na mwingine njia ya vita, hivyo kwamba ndugu mmoja alifanya
amani na Mu’awiyah ingawa alikuwa na jeshi la watu arubaini elfu, ambapo
mwingine alikwenda vitani dhidi ya Yazid na jeshi la watu chini ya mia
moja. Kwani tunaona kwamba Imamu Huseini huyu huyu, ambaye alikataa kula
kiapo cha utii kwa Yazid kwa siku mmoja, aliishi miaka kumi chini ya
utawala wa Mu’awiyah katika hali ile ile kama ndugu yake, ambaye vile
vile alivumilia kwa muda wa miaka kumi chini ya Mu’awiyah bila kumpinga.
Lazima
isemwe katika ukweli kwamba kama Imamu Hasani au Imamu Huseini
wangelipigana na Mu’awiyah wangeuliwa bila kuwepo kwa faida yoyote kwa
Uislamu. Vifo vyao vingelikuwa havina athari mbele ya sera za Mu’awiyah
ambazo kwa nje zinaonekana kwamba ni sahihi, mwanasiasa hodari ambaye
alisisitiza kuwa kwake sahaba wa Mtukufu Mtume (saw), “mwandishi wa
wahayi,” na “mjomba wa waumini,” na ambaye alitumia kila aina ya hila
iwezekanayo kuhifadhi pazia la dini kwa ajili ya utawala wake. Aidha,
kwa uwezo wake wa kuweka jukwaa kwa ajili ya kukamilisha matamanio yake
angeliweza kuwafanya wauawe na jamaa zao wenyewe na akafanya maombolezi
ya kitaifa na kutafuta kulipiza damu yao, kama vile alivyojifanya kwamba
alikuwa akilipiza kisasi kifo cha Khalifa wa tatu.
|