|
Ujumbe wa Siku ya Ashura
kutoka kwa
Ayatullah Al-Uzma Mirza Jawwad Tabrezi (Qum-Iran).
Katika Mji
mtakatifu wa Qum, Irani; Ayatullah Al-Mirza Jawwad At -Tabrezi ameelezea
rambirambi zake za dhati kwa wafuasi wa Aal-e-Muhammad (a.s.) kwa tukio
hili linalowagusa la masaibu ya Karbala.
Katika
ujumbe wake kwenye tukio la siku ya Ashura, mtukufu Ayatullah At-Tabrezi
alisema kifo cha Bwana wa Mashahidi Hazrat Aba Abdillah Al-Hussain
(a.s.) ni njia inayong’ara na itoayo mwanga kwa Waumini, wapigania
Uhuru, wanaonyanyaswa na kwa kila tabaka la jamii na pia kwa Dini na
Imani zote.
Ayatullah
alisema kuwa fundisho linalopatikana katika tukio hili la huzuni ni kuwa
ushindi kati ya Haki na Batili wakati wote upo pamoja na Haki (ukweli).
|