BUSTANI YA USEMI

 

“Yeyote awapendaye Hassan na Husein amenipenda, na yeyote anayewachukia amenichukia.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

 

“…., Allăh hujirafikisha na wale wajirafikishao na Husain yu adui wa wale walio maadui zake.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

 

Husain anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husain…”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

 

Hao (Hassan na Husain) ni maua yangu katika dunia.”(Ewe Husain), wewe u Sayyid, mwana wa Sayyid, na ndugu wa Sayyid; wewe uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu) na mwana wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu) na ndugu wa uthibitisho (wa Mwenyezi Mungu); na baba wa uthibitisho tisa ambao wa tisa wao ni Qaim wao ambaye atakuwa Al-Mahdi.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

 

Ewe mwanangu (Husain)! Mwili wako ni mwili wangu na damu yako ni damu yangu.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

 

“Ewe Mola wangu! Mpende yule ampenda Husain.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

 

“Hassan na Husain ni masayyidi wa vijana wa peponi.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

 

“Adhabu atakayoipewa yule mwuaji wa Husain huko Motoni itakuwa sawa na nusu (nzima) ya adhabu yote watakayoipewa wenye dhambi waulimwengu.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

 

“Yeyote awapendaye Hassan na Husein amenipenda, na yeyote anayewachukia amenichukia”.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

 

“Kufa kwa heshima ni bora kuliko kuishi kwa aibu”

Imăm Husain (a.s.)

 

“Kama Dini ya (Mtume) Muhammad (s.a.w.a.) haiwezi kuendelea ila kwa kukitoa mhanga kichwa changu, basi upanga na uje ukichukue.”

Imăm Husain (a.s.)

 

Imăm Hassan na Imăm Husain (a.s.) wameuhurisha Uislamu kutokana na utumwa wa wafalme na hivyo basi, wameuhifadhi kutokana na uharibifu daima. wafalme watakuja, na wafalme watakwenda, lakini Uislamu utadumu milele. Kwa Uislamu, majina matakatifu ya Hassan na Husain yataangaza milele.

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a.)

 

Katika mambo yenye kunikesheza na kuzifanya nyeupe nywele zangu ni huzuni na misiba ya kilimwengu.

Imăm  Shafii (r.a.)

 

Huzuni yangu imenirudia na moyo wangu unahuzuni. Jicho langu halifumbi wala usingizi siujuwi.

Imăm  Shafii (r.a.)

 

Kwa sababu ya Ahli-Bayt ya Mtume (s.a.w.a.), Ulimwengu mzima ulitetema na majabali na milima ilikaribia kuyayuka.

Imăm  Shafii (r.a.)

 

 

 

Ni nani atakae mfikizia Hussein ujumbe wangu na hata kama nyoyo zatukia?

Imăm  Shafii (r.a.)

 

Hussein! Aliuliwa shahidi pasi na makosa yoyote na kanzu yake ikatapakazwa wekundu.

Imăm  Shafii (r.a.)

 

Twamuombea rehma Mtume katika ukoo wa Hashim na twawaudhi wanawe; hakika jambo hilo ni lenye kustaajabisha.

Imăm  Shafii (r.a.)

 

Ikiwa dhambi zangu ni kuwapenda watoto wa Mtume Mohammad (s.a.w.) basi ni dhambi ambazo sitatubiya.

Imăm  Shafii (r.a.)

 

Kuwa ni wao ndio watakao nishufaiya siku ya kufufuliwa na hisabu, na mwenye kuwabugudhi wao ni wenye dhambi kwa Shafii.

Imăm Shafii (r.a.)

 

Husain ni Mfalme (ni Bwana) Husain ni Mfalme wa Wafalme (ni Bwana wa Mabwana); Husain ni Dini, Husain ndiye mhifadhi wa Dini. Kichwa alikitoa, bali hakutoa mkono wake juu ya mkono wa Yazid; Hakika Husain ndiye msingi wa Lailaha illallah.

Khwaja Muienuddin Chishti Ajmeri (r.a.)

 
 

Prepared by: Khoja Shia Ithna Asheri Dar es Salaam Juloos Committee 1429AH (2008)
Email us your comments, suggestions, articles, etc through the Website Coordinator: Murtaza H. Lalji